• HABARI MPYA

    Friday, January 23, 2026

    YANGA SC YATELEZA UGENINI, YACHAPWA 2-0 NA AHLY ALEXANDRIA


    TIMU ya Yanga imeteleza ugenini baada ya kuchapwa mabao 2-0 na wenyeji, Al Ahly katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika usiku huu Uwanja wa Borg El Arab Jijini Alexandria, Misri. 
    Mabao yaliyoizamisha Yanga SC leo yote yamefungwa na winga wa kushoto, Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan ‘Trézéguet’ moja kila kipindi, dakika ya 45’+3 na 75.
    Kwa ushindi huo, Al Ahly inafikisha pointi saba kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria nyumbani na sare ya 1-1 ugenini dhidi ya wenyeji, AS FAR Rabat nchini Morocco.
    Yanga wanabaki na pointi zao nne walizovuna kwenye mechi mbili za awali wakishinda 1-0 nyumbani dhidi ya FAR Rabat na sare ya bila mabao, 0-0 ugenini na JS Kabylie.
    Mchezo mwingine wa Kundi B kesho JS Kabylie watawakaribisha AS FAR Rabat Uwanja wa Hocine Aït Ahmed mjini Tizi Ouzou.
    Yanga wanarejea nyumbani kuwasubiri Al Ahly kwa mchezo wa marudiano Januari 31 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YATELEZA UGENINI, YACHAPWA 2-0 NA AHLY ALEXANDRIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top