• HABARI MPYA

    Thursday, January 29, 2026

    AZAM FC YAICHAPA. TRA UNITED 2-0 CHAMAZI


    TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
    Mshambuliaji mpya, Jean-Jacques Ngita Kamanga aliyesajiliwa dirisha hili dogo kutoka Aris Limassol alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka APEA Akrotiri, zote za Cyprus — aliiifungia bao la kwanza Azam FC dakika ya 28.
    Naye winga wa Kimataifa wa Tanzania, Iddi Suleiman Ally ‘Nado’ akaifungia bao la pili Azam FC dakika ya 70 na kuwavunja nguvu kabisa TRA United.
    Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya tano, wakati TRA United wanabaki na pointi zao 12 za mechi tisa sasa nafasi ya tisa kwenye Ligi ya timu 16.
    Baada ya mchezo huo Azam FC itasafiri kwenda Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa Kundi B Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Nairobi United ya Kenya Jumapili Uwanja wa New Amaan Complex.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA. TRA UNITED 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top