• HABARI MPYA

    Saturday, January 17, 2026

    SALAH NA MARMOUSH WAKOSA PENALTI NIGERIA YASHINDA NAFASI YA TATU AFCON


    TIMU ya Nigeria imefanikiwa kutwaa nafasi ya tatu katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kwa ushindi wa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila mabao ndani ya dakika 90 usiku huu Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
    Shujaa wa Super Eagles leo ni mlinda mlango wa Chippa United ya Afrika Kusini, Stanley Bobo Nwabali ambaye anatajwa kuwaniwa na Simba SC ya Tanzania aliyeokoa penalti mbili mfululizo za nyota wa Ligi Kuu ya England, Mohamed Salah  wa Liverpool na Omar Marmoush wa Manchester City.
    Waliofunga penalti za Mafarao wa Misri leo ni beki wa kati wa Al Ain ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ramy Rabia na kiungo Mahmoud Saber anayecheza kwa mkopo ZED kutoka Pyramids FC, zote za Misri.
    Waliofunga penalti za Super Eagles ni Akor Adams wa Sevilla ya Hispania, Moses Simon wa Paris FC ya Ufaransa, Alex Iwobi wa Fulham ya England na Ademola Lookman wa Atalanta ya Italia.
    Kipa wa Al Ahly ya Misri, Mostafa Shobeir alifungua vizuri zoezi la mikwaju ya penalti kwa kuokoa shuti la kiungo wa Lazio ya Italia, Oluwafisayo Dele-Bashiru - lakini bahati mbaya Salah na Marmoush wakakosa mfululizo penalti mbili za mwanzo za Mafarao. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAH NA MARMOUSH WAKOSA PENALTI NIGERIA YASHINDA NAFASI YA TATU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top