• HABARI MPYA

    Monday, January 26, 2026

    SIMBA SC YASAJILI WINGA MWINGINE MUIVORY COAST AMECHEZA ULAYA NA ASIA


    KLABU ya Simba imemtambulisha winga wa kushoto, Muivory Coast, Anicet Oura (26) kutoka IF Gnistan ya Finland kama mchezaji huru.
    Anicet Oura anakuja Simba kuungana tena na kocha Steve Barker ambaye awali alifanya naye kazi Stellenbosch FC nchini Afrika Kusini mwaka 2025 ambako alikwenda kucheza kwa mkopo akitokea Muaither SC ya Qatar.
    Stellenbosch FC ambao walimsajili Oura kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast Agosti mwaka 2023 ndio waliimuuza Muaither SC, kabla ya kurejea Afrika Kusini kwa mkopo.
    Timu nyingine alizowahi kuchezea Oura ni Africa Sports ya kwao, Ivory Coast, Lori Vanadzor na Masis za Armenia.


    Oura anakuwa mchezaji mpya wa sita Simba SC baada ya kipa Mahamadou Tanja Djibrilla Kassali Djibo (29) kutoka AS FAN Niamey ya kwao, Niger na beki wa kushoto mzawa, Nickson Clement Kibabage (25) kutoka Singida Black Stars ya nyumbani,
    Wengine ni beki wa kati, Ismaël Olivier Touré (28) kutoka FC Baniyas ya Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), winga wa kushoto Msenegal, Libasse Gueye (22) kutoka Teungueth FC ya kwao na kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chama kutoka Singida Black Stars.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI WINGA MWINGINE MUIVORY COAST AMECHEZA ULAYA NA ASIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top