TIMU ya Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Winga Mkongo, Elie Mpanzu Kibisawala alianza kuifungia Simba SC dakika ya 19, kabla ya kiungo mshambuliaji, Fredrick Magata kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 60.
Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 13 katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya nne, ikiizidi tu wastani wa mabao Mashujaa FC ambayo hata hivyo imecheza mechi tatu zaidi.
Kwa upande wao Mtibwa Sugar baada ya sare ya leo wanafikisha pointi 11 katika mchezo wa tisa nafasi ya nane.



.png)
0 comments:
Post a Comment