TIMU ya Senegal imekuwa ya kwanza kukata tiketi ya Robo Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan usiku wa leo Uwanja wa Tangier Grand mjini Tangier nchini Morocco.
Kiungo wa Villarreal ya Hispania, Pape Alassane Gueye mzaliwa wa Montreuil, Ufaransa amefunga mabao mawili dakika ya 29 na 45’+3, kabla ya mshambuliaji Ibrahim Mbaye wa Paris Saint-Germain ya Ufaransa alikozaliwa pia kufunga la tatu dakika ya 77.
Bao pekee la Sudan ambalo ndilo lilikuwa la kwanza katika mchezo wa leo limefumgwa na mshambuliaji wa Avondale FC ya Australia, Aamir Yunis Abdallah dakika ya sita tu.
Sasa Senegal inamsubiri mshindi wa mechi nyingine ya Hatua ya 16 Bora kati ya Mali na Tunisia zinazomenyana muda huu Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca ikutane naye katika Robo Fainali.



.png)
0 comments:
Post a Comment