MRENO Ruben Amorim ameacha nafasi yake kama Kocha Mkuu wa Manchester United, huku Mscotland, Darren Fletcher akiteuliwa kuwa Kicha wa muda.
Ruben alijiunga na Man United Novemba mwaka 2024 na aliiwezesha timu hiyo kufika Fainali ya UEFA Europa League huko Bilbao, Hispania mwezi Mei mwaka jana.
Huku Manchester United ikiwa katika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu, uongozi wa klabu hiyo umefanya uamuzi bila kusita kwamba ni wakati mwafaka wa kufanya mabadiliko.
Uamuzi huo unatarajiwa kuipa timu hiyo fursa nzuri ya kumaliza Ligi Kuu kwa kiwango cha juu zaidi.
Klabu hiyo imemshukuru Ruben kwa mchango wake kwa klabu hiyo na kumtakia kila la kheri kwa siku zijazo.
Mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Darren Fletcher amepewa jukumu la kuiongoza timu katika mchezo dhidi ya Burnley Jumatano.



.png)
0 comments:
Post a Comment