KLABU ya Al Ahly imemsimamisha winga wake hatari, Emam Ashour Metwally Abdelghany kwa wiki mbili na kumtoza Faini ya Pauni za Uingereza Milioni 1.5 kwa utovu wa nidhamu.
Ni tukio la muda mfupi kabla ya timu kuondoka Cairo mapema leo kuanza safari ya kuja Tanzania kwa ajili ya mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Yanga SC Jumamosi wiki hii Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Awali Emam Ashour alijumuishwa kwenye kikosi cha Al Ahly kinachokuja kucheza na Yanga, lakini hakuonekana Uwanja wa Ndege wakati timu inaondoka na ndipo taarifa za kusimamishwa zikafuatia.
“Emam Ashour alipigwa faini ya pauni milioni 1.5 za Misri, akasimamishwa kwa wiki mbili, na akaamriwa kufanya mazoezi peke yake,” imesema taarifa rasmi ya Al Ahly.





.png)
0 comments:
Post a Comment