MABINGWA watetezi, Ivory Coast wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burkina Faso usiku huu Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco.
Mabao ya Tembo yamefungwa na mawinga, Amad Diallo wa Manchester United ya England dakika ya 20, Yan Diomande wa RB Leipzig ya Ujerumani dakika ya 32 na Bazoumana Touré wa TSG Hoffenheim ya Ujerumani pia dakika ya 87.
Ivory Coast sasa itakutana na Misri katika Robo Fainali Januari 10 Uwanja wa Adrar Jijini Agadir, siku ambayo pia Algeria itamenyana na Nigeria katika Robo nyingine Uwanja wa Marrakech.
Robo nyingine zitatangulia Januari 9 kati ya Mali na Senegal Uwanja wa Tangier Grand mjini Tangier na Cameroon dhidi ya wenyeji, Morocco Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.



.png)
0 comments:
Post a Comment