BODI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeliadhibu Shirikisho la Soka la Senegal (FSF), Shirikisho la Soka la Marocco (FRMF) na wachezaji na Maafisa kadhaa kwa matukio tofauti ya utovu wa nidhamu wakati wa Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.
Bodi ya Nidhamu ya CAF imechukua hatua zifuatazo:
(1). Shirikisho la Soka Senegal (FSF), Bodi ya Nidhamu ya CAF iliamua:
Kumsimamisha Kocha Mkuu wa Senegal, Pape Bouna Thiaw kwa mechi tano (5) rasmi za CAF kwa mwenendo wake usio wa kimichezo kinyume na kanuni za Kanuni ya Nidhamu ya CAF za uchezaji wa haki na uadilifu na kwa kuuchafua mchezo.
Pape Bouna Thiaw pia ametozwa faini ya dola za Kimarekani 100,000.
Mchezaji wa Senegal, Iliman Cheikh Baroy Ndiaye amefungiwa mechi mbili (2) rasmi za CAF, kwa tabia yake isiyo ya kimichezo dhidi ya mwamuzi.
Mchezaji wa Senegal, Ismaila Sarr amefungiwa mechi mbili (2) rasmi za CAF kwa tabia yake isiyo ya kimichezo dhidi ya mwamuzi.
FSF imetozwa Faini ya dola 300,000 kwa tabia mbaya ya mashabiki wake, ambayo ilitia doa mchezo na ni kinyume na kanuni za Nidhamu za CAF za mchezo wa haki na uadilifu.
FSF imetozwa Faini dola 300,000 kwa tabia mbaya ya wachezaji wake hao, Maafisa na mashabiki wake.
FSFi imetozwa Faini ya dola 15,000 kwa utovu wa nidhamu wa Timu yake ya Taifa, kutokana na wachezaji wake watano (5) kuonyeshwa kadi za njano.
(2). Kuhusu Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF), Bodi ya Nidhamu ya CAF iliamua:
Nahodha wa Morocco, Achraf Hakimi amefungiwa mechi mbili (2) rasmi za CAF, huku mechi moja (1) hizi zikisimamishwa kwa mwaka mmoja (1) kuanzia tarehe ya uamuzi huu, kwa tabia yake isiyo ya kimichezo.
Mchezaji mwingine wa Morocco, Ismaël Saibari amefungiwa mechi tatu (3) rasmi za CAF kwa tabia yake isiyo ya kimichezo na kutozwa faini ya dola 100,000.
FRMF imetozwa Faini ya dola 200,000, kwa tabia isiyofaa ya wachezaji wa mpira wa uwanjani wakati wa mechi iliyotajwa hapo juu na dola 100,000 nyingine kwa kwa utovu wa nidhamu wa wachezaji wao hao na Maafisa wa Benchi la Ufundi waliovamia eneo la ukaguzi wa VAR na kuzuia kazi ya mwamuzi, kinyume na kanuni za uchezaji wa haki na uadilifu, kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 82 na 83 cha Kanuni za Nidhamu za CAF.
FRMF pia imetozwa faini ya dola 15,000 kwa kosa la mashabiki wake kumulika tochi za mwanga wa rangi kuwavuruga wachezaji wa Senegal wakati wa mechi.
(3). Aidha, Bodi ya Nidhamu ya CAF imetupilia mbali kesi ya tuhuma zilizowasilishwa na FRMF kuituhumu FSF kukiuka Kifungu cha 82 na 84 cha Kanuni za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2025 Morocco.



.png)
0 comments:
Post a Comment