TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Bao pekee la Dodoma Jiji FC katika mchezo wa leo limefungwa na mshambuliaji William Edgar aliyesajiliwa msimu huu kutoka Fountain Gate FC dakika ya tatu tu ya mchezo huo.
Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 10 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya 10, wakati Tanzania Prisons wanabaki na pointi zao saba za mechi nane sasa nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16.


.png)
0 comments:
Post a Comment