TIMU ya Algeria imefanikiwa kwenda Robo Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya ushindi wa bao 1-0 dhid ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) usku huu Uwanja wa Moulay Hassan Jijini Rabat nchini Morocco.
Mchezo huo ulilazimika kwenda hadi dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana — na bao pekee la Algeria ‘The Greens’ au The Desert Warriors’ limefungwa na kiungo wa Al-Duhail ya Qatar, Adil Boulbina dakika ya 119.
Algeria sasa itakutana na mshindi wa mchezo wa mwisho wa Hatua ya 16 Bora kati ya Ivory Coast na Burkina Faso zinazomenya usiku huu Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech.



.png)
0 comments:
Post a Comment