• HABARI MPYA

    Saturday, January 24, 2026

    SIMBA SC YACHAPWA KIMOJA NA ESPERANCE TUNISIA


    TIMU ya Simba imeendelea kusuasua katika Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji, Espérance katika mchezo wa Kundi D usiku huu Uwanja wa Hammadi Agrebi Jijini Tunis nchini Tunisia.
    Bao pekee la Esperance lililoizamisha Simba SC limefungwa na winga chipukizi wa umri wa miaka 19 wa Burkina Faso, Jack Diarra dakika ya 21 akimtungua kipa wa Kimataifa wa Niger, Mahamadou Tanja Djibrilla Kassali Djibo.
    Kwa matokeo hayo, Simba SC inakamilisha mechi tatu bila pointi hata moja kufuatia kufungwa mechi mbili za awali pia, 1-0 nyumbani na Petro de Luanda ya Angola na 2-1 na Stade Malien nchini Mali.
    Kwa upande wao Esperance wanashinda mechi ya kwanza Kundi C kufuatia sare za 0-0 na Stade Malien nyumbani na 1-1 na Petro de Luanda nchini Angola.
    Simba SC wanarejea nyumbani kuwasubiri Espérance de Tunis kwa mchezo wa marudiano Februari 1 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kutafuta ushindi wa kwanza hatua ya makundi.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YACHAPWA KIMOJA NA ESPERANCE TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top