• HABARI MPYA

    Sunday, January 18, 2026

    YANGA SC YAMSAJILI KIPA ALIYEIFAKIA STARS DHIDI YA TUNISIA NA MOROCCO AFCON


    KLABU ya Yanga imemtambulisha kipa Hussein Masalanga (33) kuwa mchezaji wake mpya dirisha hili dogo akijiunga na Wananchi kutoka Singida Black Stars (33).
    Yanga imevutiwa na Masalanga baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco.
    Masalanga alidaka mechi mbili ngumu, ya mwisho ya Kundi C Tanzania ikitoa sare ya 1-1 na Tunisia Desemba 30 na ya Hatua ya 16 Bora Taifa Stars ikifungwa 1-0 na wenyeji, Morocco.
    Anakuwa mchezaji mpya wa tano Yanga dirisha hili dogo na wa pili tu mzawa, baada ya mshambuliaji Emmanuel Mwanengo kutoka TRA United ya Tabora.
    Wengine wapya ni kiungo Mguinea Mohamed Damaro Camara kutoka Singida Black Stars aliyechukua uraia wa Tanzania, winga Mganda Allan Okello kutoka Vipers ya kwao na mshambuliaji, Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depú’ kutoka Radomiak Radom ya Poland.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAMSAJILI KIPA ALIYEIFAKIA STARS DHIDI YA TUNISIA NA MOROCCO AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top