TIMU ya Nigeria imefanikiwa kwenda Nusu Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Algeria usiku huu Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco.
Mabao ya Super Eagles leo yamefungwa na washambuliaji, Victor James Osimhen wa Galatasaray ya Uturuki dakika ya 47 na Akor Jerome Adams wa Sevilla ya Hispania dakika ya 57.
Nigeria sasa itakutana na wenyeji, Morocco katika Nusu Fainali January 14 Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.



.png)
0 comments:
Post a Comment