TIMU ya Namungo FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Bao pekee la Namungo FC lililowaduwaza Coastal Union limefungwa na mshambuliaji Mkongo, Fabrice Ngoy wa Ngoy dakika ya 47.
Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 15 katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya nne, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake tisa za mechi 10 sasa nafasi ya 13 kwenye Ligi ya timu 16.


.png)
0 comments:
Post a Comment