• HABARI MPYA

    Sunday, January 04, 2026

    YANGA SC YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI


    VIGOGO, Yanga SC wameanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KVZ katika mchezo wa Kundi C jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Mabao ya Yanga SC yamefungwa na viungo, Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua dakika ya 31, Celestin Ecua mzaliwa wa Ivory Coast pia anayechezea timu ya taifa ya Chad dakika ya 54 na mshambuliaji mpya, Emmanuel Mwanengo aliyesajiliwa kutoka TRA United dakika ya 75.
    Ecua na Mwanengo wote walifunga mipira waliyopiga ilimbabatiza beki wa KVZ, Rahim Chikuni na kubadili mwelekeo kutinga nyavuni.
    Yanga sasa itahitaji ushindi katika mechi yake ya mwisho dhidi ya TRA United Jumanne ili kwenda Nusu Fainali. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top