• HABARI MPYA

    Monday, January 05, 2026

    MZIZE AANZA MAZOEZI YANGA IKIJIANDAA KUIVAA TRA KESHO


    MSHAMBULIAJI Clement Francis Mzize ameanza mazoezi leo visiwani Zanzibar baada ya kuwa nje tangu Septemba mwaka jana kufuatia kuumia goti.
    Yanga ipo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi na kesho watacheza mechi yao ya mwisho ya Kundi C kwa kumenyana na TRA United ya Tabora.
    Mzize alikuwa sehemu ya wachezaji waliofanya mazoezi na Yanga SC leo kujiandaa na mchezo wa kesho.
    Mzize aliumia Septemba 19 mwaka jana katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Wiliete SC nchini Angola, Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0.
    Baada ya vipimo na uchunguzi wa kina, Mzize alifanyiwa upasuaji Oktoba mwaka jana na kitakuwa kuwa nje kwa wiki nane hadi 10 ambazo zimekamilika na amerudi kazini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MZIZE AANZA MAZOEZI YANGA IKIJIANDAA KUIVAA TRA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top