• HABARI MPYA

    Friday, January 09, 2026

    SENEGAL YAICHAPA 1-0 MALI PUNGUFU NA KUITOA AFON


    TIMU ya Senegal imefanikiwa kwenda Nusu Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mali usiku huu Uwanja wa Tangier Grand Jijini Tangier nchini Morocco. 
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Everton ya England, Iliman Cheikh Baroy Ndiaye mzaliwa wa Rouen, Ufaransa dakika ya 27.
    Mali ilicheza pungufu kipindi chote cha pili baada ya kiungo wake, Yves Bissouma anayecheza Tottenham Hotspur ya England pia kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45’+3.
    Sifa kwa kipa wa Yanga SC, Djigui Diarra aliyeinusuru Mali kufungwa mabao zaidi kwa kuokoa michomo mingi ya hatari.
    Kwa matokeo hayo, Senegal imetanua rekodi yake ya wimbi la ushindi kwenye AFCON hadi mechi 16 bila kupoteza, ikishinda 11 na sare tano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SENEGAL YAICHAPA 1-0 MALI PUNGUFU NA KUITOA AFON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top