TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa 2-0 shod ya Hausang FC ya Njombe jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Tanzania katika mchezo huo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la CRDB yamefungwa na mshambuliaji Paul Peter Kasunda dakika ya 51 na kiungo Richard Daniel Maranya dakika ya 24.
Mechi nyingine za leo Hatua ya 32 Bora Kombe la CRDB — TRA United imeifunga Kijiwe Nongwa ya Songwe mabao 4-0 Uwanja wa Black Rhino, Arusha na Dodoma Jiji imeichapa African Sports ya Tanga mabao 2-0 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.



.png)
0 comments:
Post a Comment