TIMU ya Nigeria imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Msumbiji usiku wa jana Uwanja wa Fez mjini Fez nchini Morocco.
Mabao ya Super Eagles yamefungwa na washambuliaji, Ademola Lookman wa Atalanta ya Italia dakika ya 20, Victor Osimhen wa Galatasaray ya Uturuki mawili, dakika ya 25 na 47 na Akor Adams wa Sevilla ya Hispania dakika ya 75.
Nigeria sasa itakutana na Misri katika Robo Fainali ambayo jana iliitoa Benin kwa kuichapa mabao 3-1 Uwanja wa Adrar mjini Agadir.



.png)
0 comments:
Post a Comment