WENYEJI, Morocco wamefanikiwa kwenda Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Nigeria kufuatia sare ya bila mabao ndani ya dakika 120 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.
Shujaa wa Simba wa Atlasi ni kipa wa Al Hilal ya Saudi Arabia, Yacine "Bono" Bounou aliyeokoa mikwaju ya penalti ya winga wa AC Milan ya Italia, Samuel Chimerenka Chukwueze anayecheza kwa mkopo Fulham ya England na beki wa kushoto wa Olympiacos ya Ugiriki, Sopuruchukwu Bruno Onyemaechi.
Waliofunga penalti za Super Eagles ni mshambuliaji wa Trabzonspor ya Uturuki, Ebere Paul Onuachu na kiungo wa Lazio ya Italia, Oluwafisayo Faruq "Fisayo" Dele-Bashiru.
Waliofunga penalti za Morocco ni viungo, Neil Yoni El Aynaoui wa AS Roma ya Italia, Eliesse Ben Seghir wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, beki wa kulia, Achraf Hakimi Mouh wa Paris Saint-Germain ya Ufaransa na mshambuliaji, Youssef En-Nesyri wa Fenerbahçe S.K. ya Uturuki, huku mshambuliaji wa Lille ya Ufaransa, Hamza Igamane pekee akikosa.




.png)
0 comments:
Post a Comment