TIMU ya Cameroon imefanikiwa kuingia Robo Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Al Medina Jijini Rabat nchini Morocco.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Peter Waweru wa Kenya, mabao ya Simba Wasiofungika yamefungwa na beki wa kulia wa Stoke City ya England, Junior Baptiste Tchamadeu dakika ya 34 na mshambuliaji wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Christian Michel Kofane dakika ya 47, wakati la Bafana Bafana lilifungwa na mshambuliaji wa Orlando Pirates, Evidence Makgopa dakika ya 88.
Sasa Simba Wasiofungika watakutana na wenyeji, Simba wa Atlasi wa Morocco katika Robo Fainali baada ya wenyeji hao kuitoa Tanzania kwa kuichapa bao 1-0 usiku wa jana Uwanja wa Prince Moulay Abdellah hapo hapo Rabat.



.png)
0 comments:
Post a Comment