TIMU ya Yanga SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 53 akimalizia pasi maridhawa ya kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua.
Yanga SC sasa itakutana na Azam FC katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026 Jumanne ya Januari 13 Uwanja wa Gombani, Pemba.
Ikumbukwe Azam FC ilitangulia Fainali jana kwa ushindi wa 1-0 dhid ya Simba SC, bao pekee la beki Lameck Elias Lawi.



.png)
0 comments:
Post a Comment