• HABARI MPYA

    Friday, January 30, 2026

    DODOMA JIJI YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 PALE PALE ISAMUHYO


    TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Bao pekee la Dodoma Jiji FC katika mchezo wa leo limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Edgar William dakika ya 50 kwa ushindi huo wanafikisha pointi 13 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya nane kutoka ya 12.
    Kwa upande wao wenyeji, JKT Tanzania baada ya kichapo cha leo Uwanja wa nyumbani wanabaki na pointi zao 21 za mechi 13 sasa nafasi ya pili nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wanaoongoza kwa pointi zao 22 za mechi nane.   


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 PALE PALE ISAMUHYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top