• HABARI MPYA

    Thursday, January 29, 2026

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA KMC USITUMIKE KWA MECHI ZA LIGI


    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeufungia Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, maarufu kama KMC Complex, uliopo Mwenge Jijini Dar es Salaam kutotumika kwa mechi za Ligi Kuu kufuatia kupoteza sifa za kikanuni.
    Taarifa ya TFF iliyotolewa leo ikiwa na saini ya Meneja Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Clifford Mario Ndimbo imezielekeza klabu zinazotumia Uwanja huo mwingine hadi hapo KMC Complex itakapofunguliwa tena baada ya mapungufu yaliyoibainika kufanyiwa marekebisho.
    Mbali na wenye mali yao, KMC FC timu nyingine ambayo inatumia Uwanja huo rasmi kama wa nyumbani ni mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa miaka minne mfululizo, Yanga SC walioanza kuutumia msimu uliopita. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAUFUNGIA UWANJA WA KMC USITUMIKE KWA MECHI ZA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top