• HABARI MPYA

    Tuesday, January 20, 2026

    SIMBA SC YASAJILI KIPA WA NIGER


    KLABU ya Simba imemtambulisha kipa wa Kimataifa wa Niger, Mahamadou Tanja Djibrilla Kassali Djibo (29) kuwa mchezaji wake mpya dirisha hili dogo akijiunga na Wekundu hao wa Msimbazi kutoka AS FAN Niamey ya kwao.
    Anakuwa mchezaji mpya wa nne mpya kwa Simba SC dirisha hili dogo baada ya beki wa kushoto mzawa, Nickson Clement Kibabage (25) kutoka Singida Black Stars ya nyumbani, beki wa kati, Ismaël Olivier Touré (28) kutoka FC Baniyas ya Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na winga wa kushoto Msenegal, Libasse Gueye (22) kutoka Teungueth FC ya kwao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI KIPA WA NIGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top