KIPA wa Yanga SC, Djigui Diarra usiku wa jana aliokoa penalti mbili na kuiwezesha Mali kutinga Robo Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kwa ushindi wa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 na Tunisia Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Diarra aliokoa penalti za viungo Elias Achouri wa FC Copenhagen ya Denmark na Mohamed Ali Ben Romdhane wa Al Ahly ya Misri, huku, beki wa kushoto wa Nice ya Ufaransa naye pia akikosa penalti yake.
Waliofunga Penalti za Tunisia ni beki wa Espérance de Tunis ya nyumbani, Yassine Meriah na winga wa FC Augsburg ya Ujerumani, Elias Saad.
Waliofunga penalti za Mali ni washambuliaji, Lassine Sinayoko wa Auxerre ya Ufaransa, Gaoussou Diakité wa Red Bull Salzburg ya Austria anayecheza kwa mkopo Lausanne-Sport ya Uswisi, El Bilal Touré wa Atalanta ya Italia anayecheza kwa mkopo Beşiktaş ya Uturuki, huku kiungo wa Tottenham Hotspur ya England, Yves Bissouma na winga wa Fenerbahçe ya Uturuki, Nene Dorgeles wakikosa.
Awali, mshambuliaji wa Club Africain ya nyumbani, Firas Chaouat alianza kuifungia Tunisia dakika ya 88, kabla ya Sinayoko, kipaji kilichopikwa katika timu ya vijana ya Auxerre, Auxerre B.
Mali sasa itakutana na jirani zao, Senegal ambayo iliitoa Sudan kwa kuifunga mabao 3-1 Uwanja wa Tangier Grand Jijini Tangier.
Baada ya mchezo huo, Diarra alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi kwa kazi nzuri ya kuivusha Mali Robo Fainali.
.jpg)


.png)
0 comments:
Post a Comment