• HABARI MPYA

    Wednesday, January 28, 2026

    SIMBA SC YASAJILI WINGA WA KUSHOTO MKONGO ALIKUWA ANACHEZA CAMEROON


    KLABU ya Simba SC imemtambulisha kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Kongo-Brazzaville, Iñno Jospin Loemba (21) kutoka Colombe Sport ya Cameroon.
    Simba SC imenasa saini ya mchezaji huyo ikizipiku klabu za Simba SC Wydad Casablanca ya Morocco, MC Algiers ya Algeria, Al Ahly FC na Pyramids FC zote za Misri.
    Loemba alijiunga na Colombe Sport Oktoba 2024 akitokea Inter Club, baada ya awali kuchezea AS Otôho kuanzia Agosti 2022 hadi Novemba 2023 akitokea JS de Talangai, zote za kwao, Kongo-Brazzaville.
    Loemba anakuwa anakuwa mchezaji mpya wa saba Simba SC dirisha hili dogo baada ya kipa Mahamadou Tanja Djibrilla Kassali Djibo (29) kutoka AS FAN Niamey ya kwao, Niger na beki wa kushoto mzawa, Nickson Clement Kibabage (25) kutoka Singida Black Stars ya nyumbani.
    Wengine ni beki wa kati, Ismaël Olivier Touré (28) kutoka FC Baniyas ya Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), winga wa kushoto Msenegal, Libasse Gueye (22) kutoka Teungueth FC ya kwao, winga wa kushoto, Muivory Coast, Anicet Oura (26) kutoka IF Gnistan ya Finland na kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chama kutoka Singida Black Stars.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI WINGA WA KUSHOTO MKONGO ALIKUWA ANACHEZA CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top