TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma .
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na mshambuliaji George Chota dakika ya 21 na kiungo Said Ally Mkopi dakika ya 64, wakati la Mbeya City limefungwa na mshambuliaji Eliud Ambokile dakika ya 45’+1.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 14 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya nne, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake nane za mechi 11 sasa nafasi ya 13.



.png)
0 comments:
Post a Comment