TIMU ya Barcelona imefanikiwa kutwaa taji la Super Cup ya Hispania baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Real Madrid usiku wa jana Uwanja wa King Abdullah Sports City Jijini Jeddah, Saudi Arabia.
Mabao ya Barcelona yamefungwa na washambuliaji, Mbrazil Raphael Dias Belloli ‘Raphinha’ mawili dakika ya 36 na 73 na Mpoland, Robert Lewandowski dakika ya 45’+4, wakati ya Real Madrid yamefungwa na washambuliaji pia, Mbrazil Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior dakika ya 45’+2 na Mspaniola, Gonzalo García Torres dakika ya 45’+6.
Barcelona ilifika Fainali ya Super Cup ya Hispania baada ya kuitoa Athletic Bilbao kwa kuichapa 5-0 na Real Madrid ikishinda 2-1 dhidi ya ya Atlético Madrid mechi zote zikipigwa Uwanja wa King Abdullah Sports City Jijini Jeddah.



.png)
0 comments:
Post a Comment