MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mwigulu Airtel Complex, Singida.
Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Mpumelelo Dube dakika ya 39, winga Mganda, Allan Okello kwa penalti dakika ya 45’+2 na kiungo Mudathir Yahya Abbas dakika ya 56.
Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 32 katika mchezo wa 12 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya JKT Tanzania ambayo pia imecheza mechi tano zaidi.
Kwa upande wao Singida Black Stars wanabaki na pointi zao 19 za mechi 12 pia nafasi ya tisa.



.png)
0 comments:
Post a Comment