• HABARI MPYA

    Saturday, January 03, 2026

    TAIFA STARS WAZAWADIWA SH. MILIONI 500 BAADA YA KUFUZU KUTINGA 16 BORA AFCON



    SERIKALI kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameizawadia timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) shilingi milioni 500 kufuatia kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).
    Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 03, 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Taifa Stars kwa njia ya simu walipotembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda 
    Waziri Mkuu Dkt. Nchemba amesema kuwa, Mheshimiwa Rais  amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono timu hiyo.
    Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Rais Dkt. Samia ameahidi kutoa zawadi nono zaidi endapo Taifa Stars itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS WAZAWADIWA SH. MILIONI 500 BAADA YA KUFUZU KUTINGA 16 BORA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top