• HABARI MPYA

    Monday, January 05, 2026

    SALAH NA MISRI WAENDA ROBO FAINALI AFCON


    TIMU ya Misri imefanikiwa kwenda Robo Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Benin usiku huu Uwanja wa Adrar mjini Agadir nchini Morocco. 
    Dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, kiungo wa Al Ahly, Marwan Attia akianza kuifungia Misri dakika ya 69, kabla ya mshambuliaji wa Victoria Rosport ya  Luxembourg, Jodel Dossou kuisawazishia Benin dakika ya 83.
    Mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza na beki wa Al Ahly, Yasser Ibrahim akafunga bao la pili dakika ya 97, kabla ya Nahodha na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah kufungana la tatu dakika ya 120’+4.
    Misri sasa itakutana na mshindi kati ya Nigeria na Msumbiji ambazo zinamenyana muda huu katika mchezo mwingine wa Hatua ya 16 Bora Uwanja wa Fez mjini Fez. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAH NA MISRI WAENDA ROBO FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top