TIMU ya Namungo FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Nyota wa mchezo huo ni kiungo, Jacob Raymond Massawe aliyefunga mabao matatu peke yake dakika ya 11, 28 na 45, huku bao lingine likifungwa na winga Hassan Salum Kabunda dakika ya 89 baada ya Kagera Sugar kutangulia na bao la Hamisi Adam dakika ya nane.
Mechi nyingine za hatua ya 32 Bora Kombe la CRDB leo, Pamba Jiji FC imesonga mbele kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Transit Camp ya Dar es Salaam jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Nayo Geita Gold imesonga mbele kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Nyika ya Pwani jioni ya leo Uwanja wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
Mechi nyingine ya Hatua ya 32 Bora Kombe la CRDB Mashujaa FC imeitoa KegGold ya Mbeya kwa penalti 5-3 baada ya sare ya bila mabao ndani ya dakika 90 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.







.png)
0 comments:
Post a Comment