TIMU ya Yanga SC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TRA United ya Tabora usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Chad, Celestine Ecua mzaliwa wa Ivory Coast dakika ya 31 akimalizia kazi nzuri ya winga Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli.
Yanga sasa itakutana na Singida Black Stars katika Nusu Fainali, wakati watani wao, Simba SC watakutana na Azam FC.



.png)
0 comments:
Post a Comment