• HABARI MPYA

    Monday, January 05, 2026

    TUNISIA YAMFUKUZA KOCHA TRABELSI BAADA YA KUTLEWA AFCON


    KOCHA Mkuu, Sami Trabelsi ameondolewa kazini Tunisia baada ya Carthage Eagles kutolewa kwenye Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazoendelea nchini Morocco.
    Uamuzi huo umethibitishwa na Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) jana, Jumapili ndani ya saa 24 tangu Tunisia itolewe katika na Mali kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo huo a Hatia ya 16 Bora Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca.
    Katika taarifa rasmi inayoelezea hatua hiyo, shirikisho hilo lilisema uamuzi huo ulichukuliwa kwa makubaliano ya pande zote mbili na Benchi la Ufundi, likitaja kutolewa mapema kwa timu hiyo kutoka kwenye mashindano.
    "Kamati ya Utendaji imeamua kusitisha uhusiano wa kimkataba kwa ridhaa ya pande zote mbili na Benchi zima la Ufundi la timu ya taifa," Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) lilisema katika taarifa Jumapili.
    Kufukuzwa kazi huko kufuatia kuongezeka kwa hasira za umma na ukosoaji mkubwa wa utendaji wa Tunisia katika mashindano hayo, ambapo matarajio yalikuwa makubwa baada ya kuanza kwa matumaini katika hatua ya makundi.
    Tunisia ilifungua kampeni yao ya AFCON 2025 kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Uganda, matokeo ambayo yaliongeza matumaini ya mbio ndefu kwa muda mfupi.
    Hata hivyo, matumaini hayo yalipunguzwa haraka na kipigo cha 3-2 dhidi ya Nigeria, kabla ya sare ya 1-1 na Tanzania katika mechi yao ya mwisho ya makundi kuacha wasiwasi kuhusu uthabiti.
    Mashaka hayo yalifichuliwa katika Hatua ya Mtoano dhidi ya Mali, kwani licha ya kuanza kupata bao, lakini Mali ilisawazisha ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja kabla ya kwenda kushinda kwa matuta.
    Tangu ilipotwaa taji la AFCON ikiwa mwenyeji mwaka 2004, Tunisia haijaweza tena kufanya hivyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TUNISIA YAMFUKUZA KOCHA TRABELSI BAADA YA KUTLEWA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top