• HABARI MPYA

    Friday, January 30, 2026

    MBEYA CITY YABANWA NYUMBANI, SARE 1-1 NA PAMBA JIJI


    WENYEJI, Mbeya City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Kiungo Adilly Buha alianza kuifungia Mbeya City dakika ya 21, kabla ya kiungo mwingine, Kelvin Nashon Naftali kuisawazishia Pamba Jiji FC dakika ya 31.
    Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha pointi tisa katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya 14 kutoka ya 13, wakati Pamba Jiji inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya tatu kutoka ya nne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YABANWA NYUMBANI, SARE 1-1 NA PAMBA JIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top