• HABARI MPYA

    Monday, January 05, 2026

    SIMBA SC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


    TIMU ya Simba SC imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fufuni FC ya Pemba katika mchezo wa mwisho wa Kundi B usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Mabao ya Simba SC yamefungwa na beki wa kati, Hussein Ally Mbegu aliyepandishwa kutoka timu ya vijana dakika ya 23 na kiungo Mguinea, Naby Camara dakika ya 90, wakati bao pekee la Fufuni limefungwa na Mboni Steven dakika ya 15.
    Simba SC inafikisha pointi sita kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwembe Makumbi City FC kwenye mchezo wa kwanza.
    Fufuni na Mwembe Makumbi City FC zinamaliza na pointi moja kila timu kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo baina yao ambao ulikuwa ndio wa kwanza kabisa wa Kundi B hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top