• HABARI MPYA

    Wednesday, January 28, 2026

    COASTAL UNION YABANWA MBAVU NA KMC MKWAKWANI


    WENYEJI, Coastal Union wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    KMC walianza vizuri mchezo huo na kutangulia kupata bao kupitia kwa Jammy Suleiman dakika ya 45’+2, kabla ya Gradi Kiala kuisawazishia Coastal Union dakika ya 47.
    Kwa matokeo hayo, Coastal Union wanafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi 11 sasa, ingawa wanabaki nafasi ya 13 wakati KMC inafishika pointi tano katika mchezo wa 11 sasa na kuendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YABANWA MBAVU NA KMC MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top