WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya bila mabao na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons inafikisha pointi nane katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya 14 kutoka ya 15 ikiizidi tu wastani wa mabao Mbeya City ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi.
Kwa upande wao JKT Tanzania inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 11 na kurejea kileleni ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia tano mkononi.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu unaendelea hivi sasa, Mtibwa Sugar wakimenyana na Pamba Jiji Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.



.png)
0 comments:
Post a Comment