• HABARI MPYA

    Monday, January 26, 2026

    KIPA WA ZAMANI YANGA, MTIBWA SUGAR NA TAIFA STARS MANYIKA MKUBWA AFARIKI DUNIA

    Kwaheri Manyika Peter Manyika, pumzika kwa amani kipa hodari na mahiri.

    KIPA wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania, Manyika Peter Manyika (52) amefariki dunia Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam.
    Manyika ambaye ni baba wa kipa wa zamani wa Simba SC Peter Manyika Junior - mwili wake umehifadhiwa katika hospital ya Mwananyamala, Dar es Salaam huku taratibu za mazishi zikiendelea.
    Manyika aliibukia klabu ya Mtibwa Sugar akiipandisha Ligi Kuu mwaka 1996, kabla ya kuhamia Sigara FC ya Dar es Salaam ambako alidumu kwa msimu mmoja, 1997.
    Huyu ni mwanawe, Peter Manyika ambaye alidakia kwa mahasimu, Simba SC

    Akiwa Sigara aliiponza timu hiyo kushushwa Daraja baada ya kupokwa pointi za mechi zote alizodaka kwa sababu ya ukiukwaji wa taratibu za usajili wake kutoka Mtibwa Sugar.
    Mwaka 1998 alijiunga na Yanga SC ambako aliidakia hadi mwaka 2001 alipokwenda Botswana kucheza soka ya kulipwa hadi mwaka 2004 akarejea nchini na kwenda kujiunga tena na Mtibwa Sugar alikocheza hadi mwaka 2006 alipostaafu.
    Manyika Peter kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco uliomalizika kwa sare ya 3-3 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru, Dar es Salaam
    Manyika Peter hapa Yanga ikimenyana na Zamalek ya Misri katika mechi ya Kombe la Washindi Afrika liomalizika kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru, Dar es Salaam

    Manyika pia alikuwa kipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kati ya mwaka 1998 na 2002 alipopokonywa namba na Juma Kaseja.
    Baada ya kistaafu soka, pamoja na Ukocha lakini pia Manyika alikuwa anajishughulisha na muziki.
    Mungu ampumzishe kwa amani. 😭
    Manyika Peter mwenye kofia kabla ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia ambao Taifa Stars ilifungwa 1-0 na Ghana mwaka 2001 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA WA ZAMANI YANGA, MTIBWA SUGAR NA TAIFA STARS MANYIKA MKUBWA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top