• HABARI MPYA

    Sunday, March 08, 2026

    AZAM FC NA SINGIDA BLACK STARS ZATINGA 16 BORA KOMBE LA CRDB

    TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini dar es Salaam.
    Bao pekee la Azam FC, moja ya timu tishio za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara lililoitupa nje Mbeya Kwanza inayoshiriki Ligi ya Championship limefungwa na winga Iddi Suleiman Ally 'Nado' dakika ya 11 akimalizia kazi nzuri ya beki wa kulia, Nathaniel Raphael Chilambo.
    Nayo Singida Black Stars imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la CRDB kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Songea United leo Uwanja wa Mwigulu Airtel Complex mkoani Singida.
    Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na  mshambuliaji Mkenya, Elvis Rupia, kiungo Mghana, Emmanuel Kwame Keyekeh kwa penalti na mshambuliaji mwingine, Muivory Coast, Joseph Gnadou Guede.
    Nayo Mbeya City imeitoa Bandari FC kwa kuichapa 3-0 mabao ya Vitalis Mayanga dakika ya 16 na 55 na Riphat Msuya dakika ya  76 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. 
    Ilikuwa siku mbaya kwa timu mbili za Ligi Kuu, Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar ambazo zimetolewa na timu za Championship kwa vipigo vinavyofanana nyumbani, 1-0 zote.
    Mtibwa Sugar imefungwa 1-0 na Mbuni FC ya Arusha bao la Omary Athumani dakika ya 33 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, wakati Tanzania Prisons imefungwa 1-0 na TMA Stars ya Arusha pia bao la Ernest Baltazari dakika ya 39 Uwanja wa Halmashauri ya Wilaya Chunya Jijini Mbeya.
    MATOKEO YOTE 32 BORA KOMBE LA CRDB
    Azam FC 1-0 Mbeya Kwanza
    Yanga SC 7-1 Polisi Tanzania
    Singida Black Stars 3-1 Songea United
    Mbeya City 3-0 Bandari FC
    Mtibwa Sugar 0-1 Mbuni FC
    Tanzania Prisons 0-1 TMA Stars
    Fountain Gate 2-1 Gunners FC
    Coastal Union 4-1 Stand United
    Simba Sc 2-0 B19 FC
    Namungo FC 4-1 Kagera Sugar
    Pamba Jiji FC 2-1 Transit Camp
    Geita Gold 4-1 Nyika FC
    Mashujaa FC 0-0 KegGold (Penalti 5-3)
    JKT Tanzania 2-0 Hausang FC
    TRA United 4-0 Kijiwe Nongwa 
    Dodoma Jiji 2-0 African Sports
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC NA SINGIDA BLACK STARS ZATINGA 16 BORA KOMBE LA CRDB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top