• HABARI MPYA

    Sunday, January 25, 2026

    SINGIDA BLACK STARS YAWACHAPA WAKONGO 1-0 ZANZIBAR


    TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa bao 1-0 AS Otohô ya Kongo-Brazzaville katika mchezo wa Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.
    Bao pekee la Singida Black Stars limefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya, Elvis Baranga Rupia dakika ya 37.
    Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi nne na kupanda nafasi ya pili ikiizidi pointi moja AS Otohô kuelekea mchezo wa marudiano baina yao Februari 1 Uwanja wa Alphonse Massemba-Débat Jijini Brazzaville.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo utaendelea hivi sasa kati ya CR Belouizdad na Stellenbosch ya Afrika Kusini Uwanjja wa Nelson Mandela Jijini Algiers, Algeria.
    Stellenbosch ndio wanaongoza Kundi C kwa pointi zao nne, wakati CR Belouizdad ina pointi tatu sawa na Otoho kabla ya matokeo ya mchezo wao wa leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAWACHAPA WAKONGO 1-0 ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top