TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-1 dhid ya URA ya Uganda jioni ya leo katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Pongezi kwa chipukizi aliyepandishwa kutoka timu ya vijana, Alobogast Kyobya kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 90’+4 baada ya kupewa nafasi ya na Kocha muumini wa vijana katika soka, Mkongo Jean-Florent Ibenge.
URA walitangulia kwa bao la mshambuliaji mzawa, Nelson Senkatuka dakika ya 10, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jephte Kitambala Bola kuisawazishia Azam FC dakika ya 23.
Azam FC inafikisha pointi saba baada ya ushindi huo na kufuzu kama kinara wa Kundi A ikifuatia na Singida Black Stars yenye pointi tano na zote zinakwenda Nusu Fainali.
Sasa timu hizo zitasubiri washindi wa makundi B na C kukamilisha timu nne za kuwania tiketi ya Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026.



.png)
0 comments:
Post a Comment