TIMU ya Senegal imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Misri usiku huu Uwanja wa Tangier Grand Jijini Tangier nchini Morocco.
Bao pekee la Simba wa Teranga katika mchezo huo mtamu wa Nusu-Fainali AFCON 2025 limefumgwa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Sadio Mané ambaye kwa sasa anachezea Al-Nassr ya Saudi Arabia dakika ya 78.
Senegal sasa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya wenyeji, Morocco na Nigeria watakaomenyana kuanzia Saa 5:00 usiku Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.
Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah na wa Manchester City, Omar Marmoush hawakuweza kuwasaidia Mafarao kufurukuta mbele ya Simba wa Teranga.



.png)
0 comments:
Post a Comment