KLABU ya Yanga imemtambulisha winga wa kulia anaweza kukikimbia na kushoto pia, Mgambia Bubah Jammeh (27) kutoka Interclube ya Angola kuwa mchezaji wake mpya katika dirisha hili dogo.
Mchezaji huyo mwenye kipaji kikubwa pendekezo la Kocha Mreno wa timu hiyo, Pedro Valdemar Soares Gonçalves tayari yupo visiwani Zanzibar na timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa leo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inatarajiwa kushuka Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo kumenyana na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa leo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika.
Bubah Jammeh anakuwa mchezaji mpya wa sitano Yanga dirisha hili dogo baada ya kiungo Mguinea Mohamed Damaro Camara kutoka Singida Black Stars aliyechukua uraia wa Tanzania, winga Mganda Allan Okello kutoka Vipers ya kwao na mshambuliaji, Muangola - Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depú’ kutoka Radomiak Radom ya Poland.
Wengine ni wazawa wawili, kipa Hussein Masalanga (33) kutoka Singida Black Stars (33) na mshambuliaji Emmanuel Mwanengo kutoka TRA United ya Tabora.



.png)
0 comments:
Post a Comment