• HABARI MPYA

    Saturday, January 03, 2026

    SINGIDA BLACK STARS YATOA SARE 1-1 NA URA KOMBE LA MAPINDUZI


    TIMU ya Singida Black Stars imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na URA katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Beki wa kulia, Hudu Mulikyi alianza kuifungia URA dakika ya 26, kabla ya kiungo Muivory Coast, Idriss Diomande kuisawazishia Singida Black Stars dakika ya 45.
    Kiungo wa ulinzi wa Singida Black Stars, Mnigeria Morice Ugochukwu Chukwu alizawadiwa Sh. Milioni zilizotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa kuwa Mchezaji Bora wa mechi hiyo.

    Naye Hudu Mulikyi alizawadiwa Sh. 500,000 kutoka kwa wadhamini wa michuano ya mwaka huu, Benki ya NMB kwa kuwa Mchezaji mwenye Nidhamu.
    Kwa matokeo hayo, Singida Black Stars inafikisha pointi tano ndani ya mechi tatu ikishinda moja, 3-1 dhidi ya Mlandege FC na sare mbili pamoja na ya leo, nyingine ya 1-1 pia dhidi ya Azam FC.
    Kwa upande wao, URA wanafikisha pointi nne kufuatia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Mlandege FC na sasa watakamilisha mechi zao kwa kucheza na Azam FC Jumatatu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YATOA SARE 1-1 NA URA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top