KLABU ya Azam FC imethibitisha kumhamisha mshambuliaji wake chipukizi, Mohamed Shilla kwenda AIK ya Sweden kwa makubaliano ambayo hayajawekwa wazi.
“Tunayofuraha kuthibitisha kuwa tumefanya uhamisho wa mchezaji wetu wa Azam FC Youth, Mohamed Shilla kwenda klabu ya AIK ya Sweden,”imesema taarifa ya Azam FC na kuongeza;
“Tunamtakia kila la kheri kwenye safari yake mpya ya soka,”.
Shilla ni kati ya wachezaji wanne wa Akademi ya Azam FC waliopelekwa AIK kuendelezwa soka katika mpango Maalum wa ushirikiano baina ya klabu hizo — wengine ni Pius Severine, Ismail Omar na Adnan Rashid.


.png)
0 comments:
Post a Comment