MSHAMBULIAJI Lionel Messi amekubali Mkataba mpya wa kubaki Barcelona.
Nyota huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 26 maisha yake tote amechezea klabu hiyo ya Katalunya na atampiku Cristiano Ronaldo kwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani katika mkataba wake mpya.
Taarifa ya klabu imesema: "FC Barcelona imefikia makubaliano ya kurekebisha vipengele via mkataba mpya na Leo Messi katika klabu,".
Amepigwa bao: Cristiano Ronaldo sasa si mchezaji anayeongoza kwa kulipwa duniani
"Mkataba mpya unatarajiwa kusianiwa ndani ya siku chache zijazo,".
Habari hizo zinangeza moral ya Barcelona wakati wanajiandaa kwa mchezowa kesho usiku wa La Liga wa kuamua bingwa baina yao na Atletico Madrid.
0 comments:
Post a Comment